Wananchi wa visiwa vya Zanzibar wamo katika harakati za kusikiliza na kufuatilia harakati za kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba 31 mwaka huu zinazotolewa na wagombea wa vyama mbali mbali nchini.Tafauti na miaka ya nyuma ambapo kipindi kama hichi cha kampeni huambatana na fujo na ghasia za mara kwa mara ikiwamo wanachama wa vyama vya siasa kutupiana maneno ya kejeli na kupigana hadharani.
Hali hii ni matunda ya maridhianao ya kisiasa yaliyofikiwa na viongozi wa juu wa vyama hivyo Mh Dr Aman Karume wa chama cha mapinduzi na kiongozi mkuu wa upinzani hapa Zanzibar Mh Seif Sharif Hamad wa CUF,viongozi hao walikubaliana kuwaunganisha wazanzibar na kusahau tafauti zao kwa manufaa ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment